Nyumba 2 zaungua moto makangale micheweni pemba.

Na Shaaban Ali
Familia mbili tofauti ambazo zinaishi katika shehia ya makangale wilaya ya micheweni mkoa wa kaskazini pemba zimetakiwa kuwa na ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuunguliwa na moto katika nyumba zao wanazoishi.
Wito umetolewa na mkuu wa wilaya ya micheweni bw Abeid Juma Ali kwa nyakati tofauti wakati akizitembelea pamoja na kuzifariji familia hizo ambazo zimekumbwa na janga hilo.
Akizitaja familia ambazo zimepatwa na janga hilo amesema kuwa ni nyumba ya Said Usumbi Misana ambayo imeungua usiku wa tarehe 14 pamoja na nyumba ya Abeid James Malaleambayo imeungua siku ya tarehe 12 mwezi huu.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kwa kushirikiana na masheha wao kuhakikisha wanaripoti katika vyombo vya sheria pindi wanapokumbana na matatizo kama hayo ili serikali iweze kupata taarifa hizo.
Nao waathirika wa janga hilo wamewapongeza wananchi wenzao ambao wamejitokeza kwa ajili ya kuwasaidia kuuzima moto huo licha ya kwamba ulitokea majira ya usiku.

Aidha wameipongeza serikali ya wilaya ya micheweni kwa kufika katika eneo pamoja na kuwafariji na kuongeza kuwa jambo hilo ambalo limefanywa sa serikali linatia moyo kwa wananchi wake.

Comments