Mvua ianyo endelea kunyesha kote nchini bado nichangamoto kwa baadhi ya wananchi.


Zaidi ya nyumba mia tisa zimeathirika na mvua iliyonyesha usiku wa juzi kuamka jana majira saa sita usiku mpaka saa nne asubuhi huku mtu mmoja akipoteza maisha.

Kutokana na kadhia hiyo serikali ya imetangaza maakazi ya dharura kwa waathirika huku ikiagiza kamati za maafa ngazi ya shehia kuandikisha wananchi wote walioathirika.
Akitoa taarifa ya maafa yaliyosababishwa na mvua waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohd Aboud Mohd amesema kutokana na mvua hizo kuathiri kwa kiasi kikubwa wananchi wa Znz serikali pia imepanga kugawa viwanja kwa waakazi wote waliojenga mabondeni na tayari viwanja hivyo vipo huko eneo la Tunguu.
Mvua hiyo pia imesababisha upotevu wa mali na vifaa vya wakaazi wa wilaya ya mjini,magharibi A magharibi B.
Ziwa maboga watu walikuwa wanavushwa kwa shilingi 100 kutoka ziwa maboga kutoka mshelishelini hadi skuli ya tomondo.
chanzo;swahiba.

Comments