MSONGAMANO WA MAGARI CHAKECHAKE PEMBA WASABABISHA SHUGHULI ZA KIUCHUMI KUSIMAMA KWA MASAA MANNE

Shughuli za kiuchumi katika mji wa Chake chake leo zilisimama kwa muda kufuatia madereva wa magari ya abiria kuweka foleni iliyosababisha magari kushindwa kuingia na kutoka katika stendi kuu ya Chake chake kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutekeleza amri ya serikali kuegesha magari katika stendi hiyo ambayo ni finyu kieneo.
Msongamano huo uliochukuwa takriban masaa manne ulisababisha usumbufu kwa wananchi wanaokwenda katika shughuli zao mbali mbali za kijamii.

Wakizungumzia kadhia hiyo baadhi ya madereva wamesema tatizo hilo limesababishwa na ufinyu wa eneo la stendi na wingi wa magari yanayoingia katika stendi hiyo .
Katibu wa jumuiya ya madereva mkoa wa kusini Pemba (PESTA)Hafidhi Mbaraka Salim amesema chanzo cha msongamano huo wa magari ni kutekeleza agizo walilopewa kutoka katika ofisi ya mkoa na jeshi la polisi.
Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Mwanajuma Majid Abdalla amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za kazi zao za udereva ili kuepusha mizozo isiyo ya lazima .

Comments