Mikakati mipya ya kukuza kiwango cha elimu kwa wanafunzi wa mkoa wa kaskazini Pemba kuanza sasa.

BODI ya elimu Mkoa wa Kaskazini Pemba, imeandaa mikakati mipya ya kunyanyua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa skuli za Mkoa huo.
Akizungumza na walimu wakuu pamoja na walimu wakuu wasaidizi , Afisa wa Elimu na Mafunzo ya Mohamed Nassor Salim ameitaja mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuongeza kasi ya ufuatiliaji maskulini, ili kuboresha utendaji wa kazi.
Alisema, mkakati wa pili ni kuunda kamati za wataalamu wa masomo mbali mbali na kuandaa mafunzo kwa walimu wapya.
Afisa huyo akitaja mkakati wa mwengine na kusema, ni kuimarisha mfumo wa mitihani wa muhula, ili kutoa tathmini ya uelewa kwa wanafunzi huku akikiri kwamba matokeo ya ufaulu kwa watahiniwa wa Mkoa huo yameshuka ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita.
Alieleza kuwa, waliosajiliwa kufanya mitihani darasa la sita ni 4288 waliofaulu ni 141 sawa na asilimia 3.05, ambapo waliofanya darasa la saba ni 5255, waliofaulu ni 108 sawa na asilimia 2.02.
Kwa upande wa darasa la kumi walisajiliwa kufanya mitihani ni 3284, waliofaulu ni 2258 sawa na asilimia 68.7.
Waliofaulu daraja la kwanza ni tisa, daraja la pili 50, daraja la tatu ni 196, daraja la nne ni 1050 na daraja zero ni 557.

Comments