Kaya 106 katika Kijiji cha Dala, Kata ya Mvuha wilayani Morogoro, zimekumbwa na mafuriko na kuwaacha wananchi zaidi ya 300 bila makazi.
Akizungumza jana mkoani hapa, Mwenyekiti wa Kijiji cha Dala, Boi Lubegete alisema licha ya kaya 106 kukumbwa na mafuriko hayo, athari nyingine iliyojitokeza ni kuharibika kwa mazao na takriban ekari 300 zimesombwa na maji hayo ya mvua.
Mwenyekiti huyo alisema mvua hizo pia zimeharibu miundombinu ya barabara.
“Serikali ya kijiji inaendelea kufanya tathmini ya uharibifu wa mazao,” alisema Lubegete.
Wakazi wa eneo hilo, Kefas Yusuph na Halima Mohamed walisema mafuriko hayo yamewarudisha nyuma kimaendeleo kwa sababu wamepoteza vyakula na mifugo pamoja na nyumba zao kubomoka.
Mkazi mwingine, Halima Mohamed alisema maji hayo yamesomba samani zake zote za ndani na vyakula. “Sijui tutaishi vipi, hatuna chakula hata tone,” alisema Mohamed.
Wakazi hao wameiomba Serikali kuwapatia misaada ya haraka ya kibinadamu yakiwamo mahema, vyakula na dawa za kuzuia magonjwa ya mlipuko.
Mafuriko ya Kilosa
Zaidi ya kaya 350 katika Kijiji cha Mambegwa Kata ya Msowero wilayani Kilosa, zimehifadhiwa katika Shule ya Msingi Mambegwa baada ya nyumba zao kubomolewa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Morogoro.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana kijijini hapo, waathirika hao walisema mvua hizo zilianza kunyesha Aprili 19 zikiambatana na upepo mkali ulioangusha baadhi ya nyumba za wanakijiji na nyingine kusombwa na maji.
Walisema pia zilisababisha baadhi ya nyumba kujaa maji.
Mmoja wa waathirika, Lucy Cosmas alisema hana chakula cha kulisha familia yake, hali inayompatia wakati mgumu. “Tunashindwa hata kwenda shambani kutokana na maeneo yote ya kijiji kujaa maji,” alisema Cosmas.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mambegwa, Said Ally alisema kaya zaidi ya 355 hazina mahali salama pa kuishi na mvua bado zinaendelea kunyesha.

CHANZO;darwaya.com.
Comments