Bei ndogo ya zao la mwani ni pigo kwa wakulima Kisiwani Pemba.

Na Hamad Khatib - Micheweni.


Wakulima wa zao la mwani Kisiwani Pemba wamelalamikia  juu ya kushuka kwa  bei ya zao hilo kutoka shilling 700 Hadi sh/300 jambo ambalo linarudish nyuma maendeleo yao.
Wakizungumza na Nocomped Community Media wakulima haoa wamesema  bei hiyo ni ndogo na  haikidhi mahitaji yao kutokana na ugumu wa kazi wanayoipata ya uzalishaji wa zao hilo.
Bi Kaije Bakari Mbwana na Sharif Shoka Ismail wote wakaazi wa Wilya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wamesema kuwa kazi ya kilimo cha mwani ni kazi mzito, ambacho wakulima wanatumia nguvu nyingi, pamoja na  pesa nyingi kwa ajili ya kutafuta vifaa vya kuendeshea shughuli za kilimo hicho.
“Tunatumia nguvu, pesa zetu, na hata akilipia lakini kila siku zikisonga mbele na bei ina pungua mwanzo tukiuza  shilling 700 lakin sasa ni 300 ni hali yakushangaza kwakweli”.
Hatahivyo wakulima hao wamesema kua hawajajua sababu ya kushuka kwa zao hilo kwani mashamba yao kwa sasa wameimarika na kustawi.

“Sisi tunashangaa kadri tunavyo zalisha mwani kwa wingi ndio unapozidi kushuka bei sasa hatujui tatizo likowapi malizetu zinapotea maana tulitumia gharama kubwa kuuzalisha hadi kufikia uvunaji”.

Sambambanahayo wameiyomba serikali na makampun ya ununuz wa zao hilo kuwaongezea bei ili kuweza kujiendeleza kimaisha pamoja na kuondokana na halingumu ya kimaisha.


Comments