![]() |
baadhi ya akina mama wakiskiliza ushauri wa dr Fatma. |
Wananchi wa kijiji cha Kiuyu Mbuyun Wilaya ya Micheweni Mkoa wa
Kaskazini Pemba wameshauriwa kutumia maji yaliyowekewa dawa kwa ajili ya kuzuia
maambukizo ya maradhi ya kipindu pindu.
Wito huo umetolewa na daktar wa hospital ya kiuyu Mbuyun Fatma Juma Hariri wakati
akizungumza na wananchi hao juu ya njia za kujikinga na maradhi ya kipipndu
pindu ambacho kimekua tishio kwa wakaazi
wa kijiji hicho na hata taifa kwa ujumla.
Amesema lazima tuelewe kuwa
maradhi ya kipindu pindu ni maradhi ambayo yanasambaa zaid katika kipindi kama
hichi cha mvua, hivyo ni kufuata miongozo ya madaktar ili kuweza kunusuru
familia zeo na majanga kama hay.
“Ndungu wananchi lazima tuelewe kua kipindu pindu ni maradhi hatari
ambayo yanaweza kutuhatarishia maisha yetu hivyo hatuna budi tujikinge nayo ili
tuweze kunusuru maisha yetu.
Amesema ili kujiepusha na maradhi ya kipindu pindu nilazima jamii
kudumisha usafi wa mazingira katika maeneo yao yanayo wazunguka na kuchukua
hatua za haraka pindi wanapo hisi mmoja wao anaugua maradhi kama hayo
kumuwahisha hospitali kwa ajili kupatiwa matibabu.
![]() |
mama akichemsha maji. |
Sambamba nahayo amewataka wananchi hao tumia maji ya kuchemsha
kabla ya kunwa nay ale yalio wekewa dawa ili kuuwa vimelea vya maradhi vilivyo
ndani ya maji hayo.
Kwa upande wao wananchi wa
kijiji cha Kiuyu Mbuyuni wameahidi
kutumia vyema wito huo wa madaktar ili kuweza kunusuru vifo visivyo vitokanavyo
na maradhi hayo.
“ tume furahi sana kupata ushauri kama huu kutoka kwa wataalamu
sisi tulikua hatujui chochote juu ya kujikinga na majanga kama haya pindi
yakitokezea tunawashuku na mungu atawalipa”
Wameeleza kua ujio wa ujumbe huo wa madaktari umekuja muda muafaka
kwani utaweza kuwasaidia katika maisha yao ya sasa na yabaadae.
Comments