Amani na utulivu ni muhimu katika maisha ya wananchi.

Na Shaaban Ali
Serikali katika wilaya ya micheweniA imesema kuwa itaendelea kusimamia amani na utulivu uliopo katika jamii pamoja na kupambana na vitendo vyovyote vya hujuma vinavyoashiria kuchafuka kwa amani hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya micheweni bw Abeid Juma Ali wakati akifanya ziara katika nyumba ya sheha wa shehia ya tumbe magharibi Masoud Khamis Hamadambayo imeungua moto sehemu ya kupikia.
Katika ziara hiyo mkuu huyo wa wilaya ametoa ubani wa Tsh elfu khamsini kwa waathirika wa janga hilo ambazo zitawasaidia katika ukarabati pamoja na urudishaji wa jingo hilo.
Amesema katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi wa marudio kumekuwa kukijitokeza matukio mbali mbali ya kuhatarisha amani hivyo serikali haito wavumilia ambao wanahusika na matendo hayo.

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kuitunza amani na utulivu uliopo pamoja kuutunza usalama wao na amewaasa wananchi hao kukimbilia katika vyombo vya sheria na kutokuchukua hatua mikononi mwao pindi wanapokuwa na matatizo.

Comments