NOCOMPED COMMUNITY MEDIA

Zanzibar
Kufuatia matukiombalimbili ya uvunjifu wa amani nchini chama cha wananchi CUF kimetoa tamko juu ya hali hiyo.
Tamako hilo tolewa leo  na  kaimu mkurugenzi wa habari, uenezi na mawasiliano ya  umma Hamad Masoud Hamad ambapo amesema Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa tareh 25 Oktoba 2015, usalama wa raia wa Zanzibar na mali zao umekuwa katika hali tete.
Taarifa hiyo imesema hali hiyo  inatokana na kushuhudiwa kushamiri kwa matukio ya kuogopesha wananchi na kufurutu ada ukiukwaji wa HAKI ZA BINAADAMU miongoni mwa wananchi kunakofanywa na vyombo vilivyopewa dhamana ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi na raia wake na mali zao.
Imesema katika siku za hivi kadribuni, hususan baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Sali Jecha, kutangaza kinyume na katiba ya nchi, kufuta uchaguzi wa 25 Oktoba 2015 na matokeo yake, Zanzibar imeshuhudia uingizwaji mkubwa wa askari, vifaa na zana nzito za kivita katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Sambamba na hayo taarifa hiyo imesema kumekuwepo kwa askari wengi wa JWTZ wanaorandaranda mitaani wakiwa na silaha nzito za kivita na operasheni isiyo rasmi ya kuwakamata na kuwabambikizia kesi wananchi wasio na hatia na hatimaye kuwaweka katika vituo mbali mbali vya polisi na kuwanyima dhamana hata kwa makosa ambayo kisheria yanapaswa kudhaminiwa.
Taarifa hiyo imesema  CUF inaamini pasipo na shaka yeyote kwamba matukio ya kuchomwa moto kwa masikani na matawi ya CCM huko Pemba ama baadhi ya nyumba za watu binafsi na mali za serikali ni mambo ya kupangwa dhidi  wananchi wasio na hatia.

Katika taarifa hiyo CUF imesema  vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi vinatakiwa kakataa kuingia katika mtego wa mipango miovu ya wanasiasa wenye lengo la kuleta taharuki miongoni mwa wananchi na kuamsha hamasa na kupandisha jazba zitakazopelekea kuchafuka kwa hali ya amani ya nchi yetu. 

Comments