- Get link
- X
- Other Apps
NATO yajiingiza mzozo wa wakimbizi Ulaya
Shirika la Kujihami la NATO limetangaza kutanua operesheni zake katika kubaliana na biashara haramu ya kusafirisha wahamiaji kuingia barani Ulaya kwa kutuma meli za kivita katika bahari za Ugiriki na Uturuki.
Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ambaye anakutana na Waziri Mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu asubuhi hii mjini Brussels, amesema meli hizo zitahusika kwenye ukusanyaji taarifa, kufanya upelelezi na kushirikiana na vikosi vya ulinzi wa pwani vya Uturuki, Ugiriki na Mamlaka ya Mipaka ya Ulaya, Frontex, kuzuia biashara hiyo.
Mapema leo, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alithibitisha kuwa nchi yake inachangia meli moja ya kubebea ndege, helikopta moja na magari mawili ya ulinzi wa mpakani, kwa ajili ya operesheni hiyo.
Bahari inayoziunganisha Uturuki na Ugiriki, zote mbili zikiwa wanachama wa NATO, imekuwa lango kuu linalotumiwa na walanguzi kuvusha wahamiaji haramu wanaowania kuingia barani Ulaya.
Comments