TRA: Zanzibar kichaka cha kukwepa kod
Wakati Rais John Magufuli akipambana na wakwepa kodi ili kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa, takwimu za zinaonyesha uwapo wa wafanyabiashara wanaopitisha bidhaa za magendo kwa njia ya panya kati ya mianya 509, Zanzibar inaongoza kwa kuwa na mianya 422, huku Tanzania Bara ikiwa na mianya 87.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kuhusu mwenendo wa ukusanyaji wa mapato, matumizi ya mashine za kielektroniki katika ukusanyaji kodi (EFD), kusitishwa kwa bei elekezi na usajili wa vyombo vya moto, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, alisema bidhaa hizo hupitishwa Bandari ya Tanga na Mtwara zikitokea Zanzibar.
Alisema hali hiyo isipodhibitiwa haraka inaweza kusababisha madhara kwa sababu licha ya Bandari ya Dar es Salaam kuchangia mapato kwa kudhibiti wafanyabaishara wanaokwepa kodi katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Magufuli, bado kuna haja ya kuandaliwa mazingira rafiki yatakayowabana wakwepa kodi wanaotumia njia hizo za panya.
Alisema licha ya Bandari ya Dar es Salaam na mashine za EFDs, kuchangia kuongezeka kwa mapato, pia mamlaka hiyo imeboresha mfumo wa udhibiti wa ukwepaji kodi kwa wafanyabaishara hasa katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Magufuli.
“Mianya ya panya ni mingi na inabidi idhibitiwe haraka, tukiangalia mara moja, Zanzibar kuna mianya 422 inayopitisha bidhaa za magendo, wakati Tanzania Bara ni 87, tusiridhike na kiwango hicho kidogo ila iwekezwe nguvu kubwa kumaliza tatizo hilo,” alisema Kidata.chanzo;http://www.zanzinews.com/

Comments