NOCOMPED COMMUNITY MEDIA

PEMBA
Mkuu wa wilaya ya micheweni Abeid Juma Ali amewataka viongozi wa dini katika wilaya hiyo kutokubali nyumba za ibada kutumika kwa masuala la uvunjaji wa amani.
Amesema kuwa kila kiongozi wa dini anapaswa kusimamia na kushajihisha amani na utulivu na kuwataka wafuasi wao kuwa chanzo cha kuienzi amani iliyopo hapa nchini.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua  mkutano wa baraza la kusimamia amani  , uliofanyika katika ukumbi wa kituo cha redio jamii  micheweni , uliolenga kuienzi amani pamoja na kuilinda wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Mkuu huyo wa wilaya ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi  hao wa dini kuhakikisha kwamba  wanatumia uwezo kuzungumza na wafuasi  wao  , kujiepusha na vitendo vinavyoashiria kuwepo na uvunjifu wa amani .
Nao wajumbe wa baraza hilo wameahidi kuufikisha ujumbe kwa wafuasi wao  ili wasiwe chanzo cha kuvunja amani na utulivu.

Aidha wameviomba vyombo vya ulinzi kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria na taratibu  wakati wanapotekeleza wajibu wao ili kusiwepo na vitisho  kwa wananchi.

Comments