NOCOMPED COMMUNITY MEDIA

Korea Kaskazini yazitishia tena Marekani na K. Kusini
Kwa mara nyengine tena, Korea Kaskazini imetishia kuzishambulia Korea Kusini na Marekani kwa silaha za nyuklia, safari hii ikiwa ni baada ya nchi hizo mbili kuanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi.

Licha ya vitisho vya aina hii kuchukuliwa kuwa mbinu ya kawaida utawala wa Kim Jong Un, vinakuja katika wakati ambapo Korea Kusini inasema mazoezi ya kijeshi yaliyoanza leo na yatakayoendelea hadi mwezi ujao, ni matayarisho ya uvamizi. 
Mahusiano ambayo daima yamekuwa mabaya kati ya Korea Kaskazini, kwa upande mmoja, na Korea Kusini na Marekani, kwa upande mwengine, yamezidi kuchafuka katika siku za hivi karibuni, baada ya jaribio la nyuklia la mwezi Januari na baadaye kombora la masafa marefu la mwezi uliopita yaliyofanywa na Korea Kaskazini. 
Umoja wa Mataifa umeiwekea vikwazo vikali Korea Kaskazini, huku Korea Kusini ikionekana kuchukuwa msimamo mkali zaidi kuliko wa kawaida dhidi ya jirani yake huyo.

CHANZO;http://www.dw.com/sw/idhaa-ya-kiswahili/habari-za-ulimwengu/s-11590

Comments