Zanzibar
Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watu 20 kwa tuhuma za
kuchoma moto Nyumba, matawi ya CCM na
majengo ya huduma za jamii pamoja na waliomzomea Rais wa Zanzibar, Dk. Ali
Mohamed Shein, kisiwani Pemba.
Watu hao wamekamatwa kutokana na msako mkali unaoendelea katika mikoa miwili visiwani humo tangu
miundombinu hiyo, kuhujumiwa kwa
kuchomwa moto kwa sababu zinazodaiwa kuwa
za kisiasa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir,
alisema jana kuwa watu 20 wamekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na matukio
uchomaji moto majengo.
Alisema pamoja na kukamatwa kwa watu hao, polisi wanaendelea
kuimarisha ulinzi wa doria wa kuwasaka watu wengine na kuchunguza chanzo cha
hujuma hizo.
Matukio ya kuchomwa moto nyumba, matawi ya CCM na majengo ya
huduma za jamii, yametokea huku Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein,
akiendelea na ziara ya kikazi kisiwani Pemba.
Majengo yaliyochomwa moto yamefikia 15, zikiwamo Ofisi za CCM
katika matawi ya Tibrinzi, Kipapo, Shidi
Mkanyageni, Muambe na Kendwa.
Comments