NOCOMPED COMMUNITY MEDIA.

Umoja wa Ulaya utapendekeza utaratibu wa pamoja wa kuyashughulikia maombi ya wanaoomba hifadhi, ikiwa sehemu ya kukabiliana na wimbi kubwa kabisa la wakimbizi kulikumba bara hili tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia. 
Gazeti la Financial Times limeripoti hapo jana kwamba Kamisheni ya Umoja wa Ulaya itawasilisha pendekezo hilo kwenye mkutano wa kilele wa tarehe 17 mwezi huu, ambapo jukumu la kushughulikia maombi ya waomba hifadhi yataratibiwa na ofisi moja kuu. 
Kwa utaratibu wa sasa, waomba hifadhi hulazimika kutuma madai yao kwenye nchi ya mwanzo wanayoingia barani Ulaya, kanuni ambayo imekuwa haitekelezwi kikamilifu, baada ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani kuamua kutokuipa nguvu mwaka jana. 
Ripoti zinasema waomba hifadhi kwenye mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya walifikia milioni 1.2 mwaka jana, wengi wao wakitokea Syria, Mashariki ya Kati, na Afrika Kaskazini.

Comments