NOCOMPED COMMUNITY MEDIA

Pemba
Kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika,  kwa walimu wanaosomesha skuli ya kisiwa cha Kokota shehiya ya Mtambwe wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba, ni miongoni mwa changamoto kubwa inayo wakabili walimu hao wakati wanapokwenda kusomesha.
Walimu hao ambao wanatumia vyombo kama mashua na ngalawa za wavuvi wakati wanapokwenda kisiwani humo, imekuwa ikiwawiya vigumu kufika na kuondoka kwa wakati, licha kutumia shilingi 3000 kwa kila siku.
Akizungumza na mwaandishi wa habari mwalimu mkuu wa skuli hiyo ambae ni ni muathirika wa tataizo hilo,  Juma Ali Hamad alisema usafiri huo ambao walimu wanatumia vyombo hivyo hulazimika kukaa humo baharini kilomita 25 hadi kufika kisiwa hicho.
Alisema kuwa kutokana na kutokuwa na uhakika wa usafiri, husababisha wakati mwengine kuchelewa kuwapatia watoto haki yao ya elimu, jambo ambalo linavuru mpangilio mzima w avipindi.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma skuli hiyo, wamelalamikia uchelewaji wa waalimu wao kutokana na kukosa usafiri wa uhakika, hali ambayo huwakosesha mpangilio madhubuti wa usomeshwaji.
Mratibu wa Idara ya elimu  ya Maandalizi na Msingi Pemba Faki Sleyyum Faki alisema kuwa, katika suala hilo la usafiri kwa waalimu hao, awali walikuwa wakilipwa shilingi 60,000 na kuongezewa hadi kufika 100,000 kwa lengo la kufidia nauli.

Skuli ya kisiwa cha Kokota ambayo inawaalimu watano ambao wote wanaishi nje ya kisiwa hicho, akiwemo Mwalimu mkuu, na hulazimka kila siku kutumia usafiri wa kujitegemea wa mashuwa kwenda skulini humo.  

Comments