Pemba
Manahodha wa Vyombo vinavyovuusha wananchi kutoka Kisiwa
Panza kwenda Chokocho, wamatakiwa kuacha tabia ya kugoma kuwavuusha wananchi
kwa madai ya itikadi za kisiasa.
Hali hiyo imekuja hivi karibuni maeneo hayo kua baadhi ya
wanachi wamemadai kugomewa na kutokuvuushwa
kutoka kisiwa hicho Kwenda Chochoko, hali inayowapa shida wananchi wanaoishi
katika maeneo hayo.
Akizungumza wananchi wa kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa kusini Pemba, Mhe: Mwanajuma
Majid Abdalla alisema chombo chochote kitakacho goma kuwavusha wananchi
kitachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kukipandisha juu hadi kuozeana na hodha
wake atafikishwa kwenye vyombo vya sheria, akisema kuwa kufanya hivyo ni
kuwanyima wananchi uhuru wao.
Mh:Mwanajuma ameitaka Mamlaka ya usafiri baharini kuhakikisha
inavifutia usajili vyombo vyote vitakavyo goma kuwavusha wananchi katika kisiwa
Hicho.
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wananchi kuhakikisha wanaendelea
kudumisha amani na Utulivu uliyopo nchini, kwani wananchi wote wa kisiwa Panza
ni ndugu.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba,
Sheikhan Mohamed Sheikhan, alisema eneo la usafiri ni huru hivyo picha, rangi
na bendera zote zilizopo zinapaswa kupachuliwa, kwani maeneo huru hayana
itikadi ya vyama vyovyote vya siasa.
Kwa upande wao wananchi wa Kisiwa Panza, waliwataka manahodha
kuacha tabia ya kuwagomea kuwavuusha kwa itikadi za kisiasa kwani kufanya hivyo
ni kukiweka pabaya kisiwa Chao.
Comments