- Get link
- X
- Other Apps
Hali ya hatari imetangazwa Brussels baada ya mashambulio ya kigaidi
Idadi ya wahanga inazidi kuongezeka baada ya mashambulio ya kigaidi katika uwanja wa ndege wa Brussels na kituo cha safari za chini kwa chini za reli karibu na makao makuu ya Umoja wa Ulaya mjini humo.
Kwa mujibu wa serikali ya Ubeligiji watu 11 wameuwawa katika shambulio la uwanja wa ndege na zaidi ya 80 kujeruhiwa. Katika kituo cha safari za reli cha Maelbeek watu wasiopungua 15 wameuwawa na 55 kujeruhiwa.
Vituo vya televisheni vinazungumzia juu ya watu wasiopungua 34 waliuwawa. Sheria ya hali ya hatari imetangazwa nchini Ubeligiji.
Kwa mujibu wa ripoti za Radio za nchi hiyo msako unaendelea katika maeneo yote ya mji mkuu Brussels.
Waziri mkuu Charles Michel amesema "kimejiri kile kilichokuwa kikihofiwa".Ametangaza kuzidishwa idadi ya wanajeshi katika mji mkuu.
Vitakavyolindwa zaidi ni pamoja na mtambo wa nishati ya nuklea. Uwanja wa ndege umefungwa.
Ndege zote zilizokuwa zituwe Brussels zinageuza njia. Sehemu kubwa ya safari za reli zimesitishwa.
Hatua za usalama zimeimarishwa puia katika nchi jirani na Ubeligiji baada ya mashambulio ya kigaidi mjini Brussels.
chanzo;.dw
Comments