Nairobi Kenya: Sheria mpya ya ushuru wa magari ya mitumba yaathiri mapato

Mapato ya magari yaliotumika yanayoingia nchini Kenya yamepungua kwa zaidi ya nusu kutokana na utekelezaji wa sheria mpya ya kuongezwa ushuru.
Hali hii imeathiri pia uingizaji wa bidhaa kama vile tumbako,matunda,vyakula na hata mvinyo.
Kulingana na muungano wa waagizaji wa magari yaliyotumika Kenya,viwango vya uniti ya magari hayo yamepungua kutoka elfu 9 hadi 3 katikakipindi cha Mwezi Disemba hadi machi.
Sheria hii ilioanza kutumika Mwezi Disemba mwaka 2015 imependekeza ushuru wa shilingi laki moja na elfu hamsini kwa magari ya mitumba kutoka nchi za nje.
Shirika la kukusanya ushuru limeitetea hatua hii likilenga kukusanya mapato ya ushuru wa shilingi bilioni 25.
chanzo;cri

Comments