Uchukuzi wa umma unatarajiwa kukwama wakati huu msimu wa pasaka kufuatia halmashauri ya kitaifa ya usafiri na uchukuzi ikiendeleza msako wa magari yanayofanya kazi kinyume na sheria.
Idara ya trafiki aidha imetangazakufanya oparesheni dhidi ya magari ya umma kwa ajili ya kuimarisha usalama wa barabarani kwani idadi ya wanaosafiri wakati huu imeongezeka.
Baadhi ya kanuni zitakazozingatiwa ni kuondolewa kwa michoro,pamoja na kuhakikisha majina ya usajili wa vyama yanapatikana.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Lee Kiunjuri amesema hawataongeza muda wa kutii sheria hizo mpya na kuwataka wahudumu hao kutimiza masharti.
chanzo;cri
Comments