Kamati
ya Taifa ya kugawa ardhi ambayo inaongozwa na Kamishna wa Ardhi Bw.
Mathew Nhonge, imekutana na kukaa Juni Mosi kwa ajili ya kupitia jumla
ya maombi 45 ya kumiliki ardhi ambayo yamewasilishwa kwenye kamati
hiyo.
Katika kikao hicho, Kamati itapitia ombi moja moja na
kujiridhisha kama muombaji ama waombaji wamekidhi vigezo vya
kumilikishwa ardhi wanayoomba na kwa matumizi yaliyobainishwa kwa mujibu
wa sheria.
Kamati hii inaundwa na wajumbe ambao baadhi yao
wametajwa kwa mujibu wa sheria na wengine wanaingia kwenye kamati
kutokana na utaalam wao ndani ya sekta ya ardhi. Wajumbe
wa Kamati wanaotajwa kwa mujibu wa sheria ni pamoja na Mkurugenzi wa
Upimaji na Ramani, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi na Mipango Miji,
Mjumbe kutoka Wizara ya Afya, Maliasili na Utalii, Mifugo, Ulinzi,
pamoja na mjumbe kutoka Uwekezaji.
Kamati ya taifa ya kugawa
ardhi, inafanya kazi zake kwa mujibu wa Sheria ya ardhi Namba 4 ya Mwaka
1999 pamoja na kanuni zake ambayo imeweka bayana majukumu ya kamati na
kwamba mwenyekiti wake ni lazima awe Kamishna wa Ardhi.
Mpekuzi.
Comments