Iran, China na Russia zashauriana kuhusu mazungumzo yajayo ya JCPOA.

 Iran, China na Russia zashauriana kuhusu mazungumzo yajayo ya JCPOA 
Mwakilishi wa Russsia katika taasisi za kimataifa zenye makao mjini Vienna nchini Austria amesema kuwa jumbe za Iran, China na Russia zimejadiliana huko Vienna kuhusu hatua mazungumzo yajayo ya JCPOA. 
 
 Mikhail Ulyanov ameeleza kuwa, wajumbe za nchi tatu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, China na Russia jana Jumatatu walifanya kikao huko Vienna ambapo walijadili hali ya mambo ya sasa na njia za kuhuisha mapatano ya JCPOA. 
 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ujumbe wa Iran katika kikao hicho cha pande tatu ulieleza mitazamo na maoni yake kuhusu matini ya rasimu na masuala yaliyosalia katika mazungumzo ya Vienna. Wakati huo huo wajumbe za China na Russia pia waliwasilisha baadhi ya maoni na mapendekezo yao na kusisitiza tena kuwa nchi zao zinaunga mkono kikamilifu misimamo ya Iran.    
 
Jumbe zote tatu za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, China na Russia pia zimesisitiza kuwa zinaunga mkono kuendelezwa kazi kwa jadi bila ya  kuharakisha wala kuchelewesha.   
 
Duru ya tano ya mazungumzo ya JCPOA  ilianza Jumanne wiki iliyopita ikihudhuriwa na wawakilishi wa kundi la 4+1 huko Vienna, Austria. 
parstoday.

Comments