Wananchi watakiwa kushiriki kikamilifu kwenye maonyesho ya kilimo Pemba.


Wizara ya Kilimo maliasili Mifugo na Uvuvi Zanzibar imesema itaendelea kuyatumia maonesho kama shamba darasa kwa wajasiriamali ili waendelee kupata elimu ya shughuli wanazo zifanyanya.


Akizungumza na waandishi wa habari huko katika viwanja vya maonyesho Chamanangwe Mkoa wa Kaskazini Pemba waziri wa Wizara hiyo Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri amesema maonyesho ni njia rahisi inayo wakutanisha wajasiriamali na wadau wengine kupata elimu inayo wawezasha kujifunza mbinu mpya za kilimo, ufugaji, uvuvi nahata Nyanja nyenginezo.

Ameeleza kuwa wataendelea kuyatumia maonyesho hayo ili wananchi wapate nafasi yakujisomea kile kitakacho wasaidia katika kujiendeleza na kujikimu kimaisha na kuondokana na hali yautegemezi serekalini.

Amesema lengo la maonyesho hayo nikujitadhmini ilikuona maendeleo ya kilimo, uvuvi, ufugaji namaswala mengine kujua wapi yamefikia nakuweza kuyaendeleza.

Aidha amewasisitiza wananchi kuitikia wito wakwenda kujionea maonyesho hayo kwani nidarasa tosha ambali watajifunza kwa vitendo.

Kwaupande wake mratib wa maonyesho hayo Sharif Maalim Hamad amewatoa shaka wananchi kuwa maonyesho hayo nibure lengo nikujifunza kile ambacho watakihitaji kuweza kukijua.

Nae sheha wa shehia ya kiuyu minungwini Yahya Salim Amiir amesema wamejiandaa vyakutosha kuweza kuwapokea wageni ambao watahudhuria katika maonyesho hayo kwa salama na amani.

Maonyesho ya siku ya chakula dunia huadhimishwa kila ifikapo tarehe 16 octobar  kila mwaka kwa Zanzibar yataanza kesho ambayo kitaifa yatafanyika katika viwanja vya Chamanagwe ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzbiar Dr. Ali Mohd Shein na ujumbe wa mwaka huu ni  “matendo yetu ndio hatma yetu lishe bora kwa ulimwengu usio na njaaa”.

Comments