
Tahadhari hiyo imetolewa na TMA, ikionesha uwezekano mkubwa wa kuwepo kwa mvua kubwa sambamba na mawimbi makubwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Oktoba 9 hadi Oktoba 12, 2019.
Angalizo hilo la mawimbi Mmakubwa limetolewa pia kwa baadhi ya maeneo Pwani ya Bahari ya Hindi na kusini mwa mikoa ya Mtwara na Lindi.
Mamlaka hiyo imewataka watumiaji wa bahari na
maeneo yaliyotajwa kuchukua tahadhari.
Katika taarifa hiyo, TMA imeeleza athari kuwa kiwango kikubwa cha athari kinaweza kujitokeza.
Katika taarifa hiyo, TMA imeeleza athari kuwa kiwango kikubwa cha athari kinaweza kujitokeza.
TMA pia imeeleza athari zinazoweza kutokea ni
baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, kutawanyishwa na ucheleweshwaji wa usafiri
baharini na nchi kavu na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi
na kijamii.
Comments