Rais Magufuli akemea Ujauzito kwa Wanafunzi Rukwa.

Rais John Magufuli amewataka viongozi wa mkoa wa Rukwa, Wazazi na Walezi wote mkoani humo kushirikiana kuhakikisha wanamaliza tatizo la Mimba kwa Wanafunzi.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizungumza na Wakazi wa mkoa wa Rukwa katika mkutano wa hadhara, uliofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.
Amesema kuwa, mkoa wa Rukwa ni miongoni wa mikoa nchini yenye idadi kubwa ya Wananfunzi wanaopata Ujauzito, ambapo kwa mwaka 2018 pekee Wanafunzi 229 walipata Ujauzito.
Amesema kuwa, haiwezekani Serikali ikawa inafanya jitihada kubwa za kuendeleza Sekta ya Elimu, huku kukiwa na watu wengine wanarudisha nyuma jitihada hizo.
Amewaomba viongozi wa dini zote mkoani Rukwa kukemea suala la Ujauzito kwa Wanafunzi katika nyumba za ibada, na kuwaelekeza Wanafunzi kufuata mafundisho ya Mwenyezi Mungu na kuacha vitendo viovu.
Kwa upande wa Wanafunzi, Rais Magufuli amewataka kusoma kwa bidii na kutambua kuwa Serikali inatumia fedha nyingi ili kuboresha mazingira ya elimu, hivyo wasiichezee nafasi hiyo.

Comments