Kituo cha habari cha Tactical Report (TR) kimemnuu Ahmad bin Abdulaziz Aal Saud ambaye aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani wa Saudia akisema kuwa, kama mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo, Muhammad bin Salman ana nia ya kujiunga na na muungano wa Marekani na Uingereza katika vita dhidi ya Iran yeye atapinga wazo na fikra hiyo.
Mwanamfalme huyo ametoa wito wa kuwepo umoja kati ya nchi za Kiarabu wanachama katika Baraza la Ushirkiano wa Ghuba ya Uajemi badala ya kufuata mipango na sera za Rais Donald Trump wa Marekani ambaye amesema, analiekeza eneo la Ghuba ya Uajemi katika vita vipya.
Ahmad Bin Abdulaziz amekuwa akipinga sera za mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudia, Muhammad bin Salman na ni miongoni mwa wanamfalme wachache sana wanaowezi kueleza mimamo yao waziwazi na hadharani.
Ahmad Bin Abdulaziz ambaye ni ndugu wa baba mmoja na mfalme wa sasa wa Saudi Arabia na mjumbe katika Baraza Kuu la familia ya kifalme, alifanikiwa kuondoka nchini humo na kuelekea London nchini Uingereza masaa kadhaa tu kabla ya Bin Salman kuanza zoezi la kuwakamata na kuwafunga wanamfalme wenzake 11 Novemba mwaka 2017.
Alirejea mjini Riyadh Novemba mwaka jana. Vilevile anajulikana kwa kukosoa siasa za kaka yake yaani Mfalme wa sasa wa Saudia na vita vya nchi hiyo dhidi ya watu wa Yemen.
parstoday.
Comments