
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Takwimu za Bei Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Khamis Abdulrahman Msham, mfumko wa bei za vyakula na vinywaji visivyokuwa na vilevi ulishuka kufikia asilimia 1.8 mwezi huo wa Julai kutoka asilimia 2.4 mwezi Juni 2019.
Alisema, faharisi za bei kwa ujumla ziliongezeka hadi 110.8 mwezi Julai 2019, ikilinganishwa na 108.2 mwezi Julai 2018.
Alisema, kiwango cha mfumko wa bei za vyakula kilishuka hadi asilimia 1.8 kwa mwaka uliomalizikia Julai 2019, ikilinganishwa na asilimia 2.4 mwezi Juni 2019.
Alisema, faharisi za bei za vyakula ziliongezeka kufikia 108.3 mwezi Julai 2019 ikilinganishwa na 106.5 mwezi Julai 2018.
Kwa upande wa bidhaa zisizokuwa za vyakula, ulishuka hadi 2.8 mwezi Julai 2019 ikilinganishwa na 2.9 mwezi Juni 2019.
Alisema faharisi za bei kwa bidhaa zisizokuwa za vyakula ilifikia 112.6 mwezi Julai 2019 ikilinganishwa na 109.5 mwezi Julai 2018.
Alizitaja bidhaa zilizochangia kushuka kwa kiwango cha mwaka cha mfumko zilikuwa ni pamoja na mchele wa Mbeya (7.1%), ndizi za mtwike (26.9%), ndizi za mkono mmoja (21.2%), mafuta ya petroli (4.0), dizeli (4.6%) na mafuta ya taa (1.4%).
Kwa upande wa mfumko wa mwezi, ulishuka hadi nakisi ya 0.5 mwezi Julai 2019 ukilinganisha na 0.4 mwezi uliomalizikia Juni 2019.
Mfumko wa bei wa vyakula na vinywaji visivyo na vilevi kwa mwezi uliomalizikia Julai 2019, ulishuka hadi asilimia 1.9 ikilinganishwa na 1.0 mwezi Juni 2019.
Alisema, kushuka kwa mfumko wa bei wa mwezi ulichangiwa na bidhaa kama mafuta ya kupikia ya OKI (0.7%), ndizi za mtwike (10.8%), ndizi za mkono mmoja (9.4%), sukari nyeupe (2.9%), saruji (0.7%), mafuta ya taa (0.7%), petroli (1.6) na dizeli (0.4%).
Mkuu wa Takwimu za Kiuchumi, Abdulrauf Ramadhan Abeid, alisema, kasi ya mfumko kwa mwezi Julai kwa nchi ya Kenya ulifikia 6.27 ikilinganishwa na 5.70 wakati Uganda ulishuka hadi 2.6 kutoka asilimia 3.4.
Hata hivyo, alisema, kiujumla kasi ya mfumko kwa ukanda wa Afrika Mashariki bado ipo vizuri kutokana na kuendelea kubakia kwenye tarakimu moja.
Nae Mhadhiri wa Uchumi, kutoka Skuli ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)Dk.Suleiman Simai Msaraka,alisema, hali ya uchumi inaendelea vizuri na kinachohitajika ni kuendelea kuwepo kwa uzalishaji wa bidhaa zaidi.
Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi Benki Kuu Tawi la Zanzibar, Moto Ng’winganele Lugobi, alisema, pamoja na kasi ya mfumko huo kuongezeka, bado Zanzibar imefikia hatua nzuri kulinganisha na malengo yaliyoweka ya kuwepo kwa tarakimu moja ya mfumko wa bei kwa nchi za Afrika Mashariki.
Zanzibarleo
Comments