
Ushauri huo umetolewa na Afisa mradi wa kupinga udhalilishaji
Asha Abdallah Makame wakati wa mafunzo maalum kwa waandishi wa habri ya
kuwajengea uwezo wa kuandika habari kutoka mahakamani yaliyofanyika katika
ofisi za Tamwa chake chake Pemba .
Bi Asha amesema waandishi wengi baada ya kuandika
hawazifanyii mwendelezo habari zao hivyo amewataka kuzifuatilia kwa kina
ili kuwajuilisha wananchi namna ya kesi zinavyoendelea .
"Waandishi walio wengi huwa wanaandika habari za
udhalilishaji lakinhi shida inakuja baada ya kufika mahakamanhi watu
wanasubiri kujua kesi inaendeleajae unakuta mwenhdelezo wake haupo,niwatake
waandishi munapoandika habari basi zufuatilieni mpaka hukumu itoke hapo itakuwa
umeiridhisha jamii".amesema Asha.
Akitoa mafunzo hayo wakili wa serekali kutoka ofisi ya
mkurugenzi wa mashtaka Juma Ali Juma amesema waandishi wana dhima kubwa ya
kuhabarisha jamii juu ya mwenendo wa kesi za udhalilishaji zinavyoendelea
mahakamani .
"waandishi muna dhima kubwa, jamii inategemea kutoka kwenu
kusikia namna gani kesi zinavyoendelea pamoja na hukumu zinazotolewa"amesema
wakili Juma.
Kwa upande wao baadhi ya waandishi wamesema uwepo wa urasimu
mkubwa juu ya upatikanaji wa taarifa kutoka mahakanhi nhdio sabgabgu
iliyopelekea kuwawia vigumu kupata muendelezo wa habari zao wanazozitoa.
"Kiukweli upatikanaji taarifa jinsi kesi zinavyoendelea inakuwa
shida sana unafika kwa wahusika kutaka kupata taarifa juu ya muendelezo wa kesi
kila mmoja anamtupia mpira mwenzake mara nenda kwa msemaji Wete, wakati
mwengine wanasema wao hawajapata ruhusa ya kuzungumza alimradi inakuwa shida
mpaka unaamua kuachana nayo kwa usumbufu unaoupata". wamesema waandishi.
Comments