Soko jipya la samaki kujengwa Malindi.

SERIKALI inatarajia kujenga soko la samaki katika eneo la Malindi,ambalo litakuwa na hadhi ya soko la kitalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Utekelezaji wa mradi huo tayari umeanza ambapo serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Japani kupitia Shirika la JAICA imesaini mkataba wa ujenzi wa soko hilo ambapo unatarajiwa kuanza Aprili mwaka huu na kukamilika 2020.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliaasili Mifugo na Uvuvi, Maryam Juma Abdalla, alieleza hayo wakati akizungumza na chanzo hizhi cha habari, ofisini kwake Maruhubi.
Alisema katika ujenzi huo, serikali imetoa dola milioni 1.5 na Serikali ya Japan imetoa dola milioni 7.5.
Aidha alisema kukamilika kwa mradi huo,kutatoa fursa za ajira kwa wastani wa watu 6,050.

Alitaja miongoni mwa mambo yatakayokuwemo ndani ya soko hilo ni pamoja na kituo cha kushushia samaki na vyumba vya baridi kwa ajili ya kuhifadhia samaki na mitambo ya barafu.
Aliwataka wafanyabiashara wakati utakapofika kuanza kwa ujenzi huo, kuondoka eneo hilo ili kupisha ujenzi.

Comments