Kiranjit Ahluwalia: Mwanamke aliyemchoma moto mumewe.

Kiranjit Ahluwalia
Katika majira ya kipupwe jioni mnamo mwaka 1989, Deepak Ahluwalia alishindilia pasi ya moto kwenye uso wa mkewe, nywele zake zika zikabadilika na kuwa laini.
pasi ilichoma ngozi yake wakati alipokuwa akihangaika kumshika kwa nguvu mumewe , na kuacha alama kwenye uso wake.
Kiranjit Ahluwalia anasema tukio ambalo anasema lilitokea baada ya kupitia unyanyasaji wa muongo muongo mzima mikononi mwa mumewe.
"Sikuweza kulala , nilikuwa ninalia vibaya sana. Nilikuwa katika maumivu makali, kimwili na kisaikolojia," aliiambia BBC miaka 30 baadae
"Nilitaka kumgonga. Nilitaka kumgonga kama alivyonigonga. Nilitaka kumgonga ili aweze kuhisi maumivu niliyokuwa ninayahisi . Nikufikiria zaidi. Ubongo wangu ulikuwa haufanyi kazi kabisa ."
Usiku ule, alipokuwa amelala kitandani, alimwagia miguu ya mumewe mafuta ya petroli kisha akaichoma kwa moto. Kisha alimbeba mwanae wa kiume wakatoka nje ya nyumba.
"Nilifikiri nitauchoma mguu wake, ili asiweze kunikimbiza. Nilidhani ningempa jeraha ili awe anakumbuka wakati wote kile alichofanyiwa na mkewe . Kwa hiyo kila mara anapoona mguu wake na kovu, atakuwa ananikumbuka ."
Kiranjit anasiistiza kuwa hakukusudia kumuua mumewe.
lakini siku 10 baadae, Deepak alikufa kutokana na majeraha.
Mwezi Disemba mwaka ule , Kiranjit alipatikana na hatia ya mauaji akahukumiwa kifungo cha maisha jela.
Licha ya wazazi wake wote kufariki alipokuwa na umri wa miaka 16, alisema maisha yake ya utotoni yalikuwa ni ya kupendwa sana. Akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto tisa, alitunzwa na kupendwa na kaka zake na dada zake wakubwa.
Alipokaribia miaka ishirini , hata hivyo shinikizo la kuolewa likaanza.
"Sikutaka kuolewa kwahiyo nikaenda kwa dada yangu nchini Canada. Sikutaka kuishi nchini India, kuolewa na kupata watoto kama waliokuwa nao mawifi zangu . Nilitaka kufanya kazi nipate pesa ,niishi maisha yangu mwenyewe," alisema.
Lakini lilikuwa ni jambo alilolazima kulikubali wakati dada yake wa Uingereza alipompata mwanaume wa kumfaa.
"Alikuja kuniangalia nchini Canada. Tuliongea kwa dakika kama tano na nikasema ndio. Nilifahamu fika nisingeweza kuepuka, nikalazimika kuolewa. Kwa hiyo ikawa hivyo. Uhuru wangu ukaenda ."
Akikumbuka mtizamo wake wa kwanza kwa mumewe , alismema alikuwa "mwenye wa kupendeza , mwenye sura yenye mvuto na mchangamfu " lakini hakujua ni lini angempiga.dakika moja alikuwa mzuri kama dhahabu, na dakika nyingine aligeuka na kuwa wa kutisha''.

Anasema unyanyasaji wake ulianza siku ya kwanza tu waliooana.

"Alikuwa kama amekasirika, ni hivyo ," alisema. "Kufoka, matusi, kutupa vitu, kunisukuma, kunitisha kwa visu. Kwa hiyo mara nyingi alikuwa ananikaba shingo. Nilikuwa naachwa na maumivu na alama za kuumia na kushindwa kuongea kwa siku kadhaa.
"Nakumbuka ilikuwa ni siku yake ya kumbukuambu ya kuzaliwa kwake na nilikuwa nafanya kazi ya ziada na nikamnunulia pete ya dhahabukama zawadi yake ya siku hiyo. Wiki hiyo hiyo alikasirika akatumia pete hiyo hiyo kuvunja jino langu. Alinipiga ngumi usoni."
Kiranjit anasema kuwa kila wakati alipokuwa anajaribu kumuacha, mumewe alikuwa anamtafuta, kumrejesha nyumbani na kumpiga.
Miaka mitano ya ndoa yao, wawili hao walisafiri kutembea India ambako Kiranjit alimwambia kaka yake mateso anayoyapitia . mwanzo familia yake ilikasirika, lakini baada ya mumewe kuomba msamaha walimshawishi kurejea nyumbani kwake.
Miezi michache baadae waliporudi Uingereza, matusi yakaanza tena.
Deepak akaanza kuwa na wapenzi nje ya ndoa na kudai pesa kutoka kwa mke wake - jambo lililosababisha malumbano.
"Sikuweza kukwepa, sikuweza kupata talaka. Kulikuwa na shinikizo la familia la kuwa na mtoto. Kila mtu alisema ukiwa na mtoto labda atabadilika. Atakuwa mwanamume anayewajibika.
"Hakubadilika. Alikuwa mbaya zaidi."
Wakati Kiranjit alipokabiliwa na kesi ya mauaji ya mumewe, alisema hoja yake ya kwamba aliumizwa na mateso ya mumewe haikusikilizwa , na alihisi kukasika alipokuwa akisikia hukumu yake.
Waendeshamashtaka walisema alichochewa na wivu kwasababu mumewe alikuwa na wapenzi nje ya ndoa, na muda utofauti kati ya madai yake yake na ulipizaji kisasi ilikuwa mkubwa kiasi cha kumfanya atulie na kufikiria juu ya athari za matendo yake
"Nilikuw ana imani kubwa na sheria ya Uingereza . Nilifikiri sheria ya Uingereza ilikuwa ni ya kisasa na kwamba wangenielewa , ni kwa kiasi gani niliumia. Hawakuelewa ni miaka mingapi niliyoumia ."Kiranjit Ahluwalia akiwa nyumbani kwake
Wakati alipokuwa gerezani, Kiranjit anasema alihisi kuwa huru, mbali na mume wangu.
Alicheza badminton, akafanya masomo ya kiingereza na hata akashiriki katika uandishi wa kitabu , ambacho baadae kilitumiwa kutengeneza filamu juu ya maisha yake.
kesi yake ilichukuliwa na Southall Black Sisters (SBS), shirika linalowatetea wanawake weusi na wa jamii ya Asia.
" Tulijaribu kuzungumza na mawakali wakati huo na kujaribu kuwaelimisha juu ya muktadha wa utamaduni. Ni kwanini kwa mtu kama yeye isingekuwa rahisi kuondoka kwenye ndoa yenye mateso ," alisema Pragna Patel mkurugenzi wa shirika hilo..
Pia ilituma ujumbe kwamba wanawake wanaoua kutokana na unyanyasaji mkubwa wa nyumbani hawapaswi kuchukuliwa kama wauaji wasio hisia.
"Tuliweza kubadili kudhibiti mitizamo katika jamii zetu ," alisema Pragna . "Watu walimkubali Kiranjit na kumuona kama shujaa badala ya kumumchukia na kumtenga.
" Kipindi hicho kilikuwa muhimu katika vita vya wanawake dhidi ya unyanyasaji katika nchi hii , hususani katika mahusiano ya wanawake katika jamii za walio wachache , kukubali na kutambua kuwa unyanyasaji wa kijinsia upo na kwamba jinsi tunavyowafanyia wanawake ni moja ya sababu ya kufanyika kwa matukio kama hayo."
Rufaa ya Kiranjit imebaki kuwa inayokumbukwa sana katika kesi za shirika la SBS tangu lilipoanzishwa miaka 40 iliyopita.Kama kundi shirika linaathimisha siku ya kuasisiwa kwake, lilitengeneza filamu inayozungumzia kesi , iliyoitwa Alichochewa(Provoked), wikendi hii kama sehemu tamasha la waingereza wenye asili ya Asia Uitakayoonyeshwa kote nchini hadi Mei.
Pragna anasema suala ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake katika jamii za walio wachache bado haujapungua . Na badala yake anasema, umeongezeka.
"Ikiwa kuongezeka kwake kumesababishwa na ongezeko la watu wanaoripoti maisha yao ya unyanyasaji au ni kwasababu matukio yenyewe yameongezeka ni swali gumu kujibu ."Kiranjit Ahluwalia (wapili kutoka kushoto) akiwa ameshika mikono ya Pragna Patel (wa pili kutoka kulia ) mara baada ya kuachiliwa huru gerezani

Comments