Wizara ya Elimu Zanzibar yaonya ujenzi chini ya kiwango.

Image may contain: 2 people, people standing and outdoor
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Pembe Juma amesema serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohamed Shein haipo tayari kuona majengo ya serikali yanajengwa chini ya kiwango.
Akizungumza wakati alipofanya ziara ya kushtukiza kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Amali Makunduchi na skuli ya sekondari Kibuteni, alisema mawakala wa majengo ya Zanzibar, ZBA wapo kwa lengo kuthibitisha ubora wa mejengo yanayojengwa.
Alisema endapo itatokea wakala hao wakibaini kuwa yapo majengo yamejengwa chini ya kiwango serikali itachukua hatua za kisheria dhidi ya kampuni iliyohusika na ujenzi wa majengo husika.
Waziri huyo alisema lengo la serikali katika kujenga skuli pamoja na vyuo vya amali ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira salama na yenye utulivu.
Aidha aliwataka wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa majengo hayo kuhakikisha wanamaliza kwa wakati walikubaliana pamoja na majengo wanayoyajenga yanakua katika viwango vilivyo bora ili kuepusha usumbufu.
Nae mkandarasi Omar Hashim Mfangavo wa kampuni ya Mindset Techniques Ltd, inayosimamia ujenzi wa Chuo cha Amali Makunduchi alisema tatizo la upatikanaji mchanga nchini limechangia kuchelewa kumalizika kwa majengo hayo ambapo ameahidi kuendelea na ujenzi ili kumaliza kwa wakati.
Kwa upande wake mkandarasi, Seif Sleyum Seif kutoka kampuni ya Rans. Co.Ltd anaesimamia ujenzi wa skuli ya sekondari Kibuteni alisema hali ya ujenzi wa skuli hiyo ipo vizuri.
Mkandarasi huyo aliahidi kuyakabidhi majengo hayo mapema Juni mwaka huu bada ya kukamilika ujenzi huo.Image may contain: 4 people, people standing

Comments