Wanao kwamisha harakati za maendeleo kukiona chamoto


Image result for manga mjengo mwajiri
Waziri wa Kilimo Maliasili mifugo na uvuvi zanzibar, Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri, amesema hataweza kumnyamazia mtumishi yoyote wa wizara yake alieshiriki kudhorotesha shughuli za miradi katika kuwasaidia wananchi.

Mh. Mmanga ameyasema hayo huko katika bonde la umwagiliaji machigini, wilaya ya mkoani, mkoa wa kusini pemba.

Amesema kuwa, kuna baadhi ya watendaji wamekuwa wakisimamia miradi yao kipindi cha mwisho cha mkataba kwa malengo ya kufanya ubabaifu huku huduma zikisuasua bila maelezo yamsingi.

Amesema, kwa sasa wananchi wamehamasika kuendeleza shughuli za kilimo hakuna haja ya kuwasumbua na kuwapa sababu zisizo na msingi na kufanya ujanja na badala yake kuwapatia teknolojia za kutosha kulingana wakati ,ili waweze kupata tija.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa kuongeza tija kwa wakulima (ERPP) katika bonde la machigini afisa mkuu idara ya umwagiliaji, Mbarouk Ali Mgau, amesema ni kipindi cha miezi sasa tokea kukamilisha malipo kwa shirika la umeme lakini bado hawajapatiwa huduma, hali inayodhorotesha shughuli za   wakulima wa bonde hilo.

Kwa upande wao wakulima wa bonde hilo, wamesema kuwa, kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na tatizo la umeme ambao ungaliwasaidia katika kuvutia maji ndani ya bonde lao pamoja na ubovu wa miundombinu ya umwagiliaji.

Comments