Wananchi Kisiwani Pemba waaswa kutofanya shughuli za kimaendeleo katika maeneo tengefu.


Image result for pemba island map
Serikali imewataka wananchi kuacha kujenga nyumba au kupanda miti ya kudumu katika maeneo ambayo yametengwa kwa uwekezaji.

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti huko CHAMANANGWE na MICHEWENI na waziri wa ardhi nyumba maji na nishati Salama Aboud Talib chini ya jopo la mawaziri wanne waliotumwa na Serikali kushughulikia mizozo ya wananchi waliojenga na kupanda miti ya kudumu katika maeneo ya uwekezaji.

Mheshimiwa Salama amesema ifikie wakati wananchi kutambua kwamba maeneo ya uwekezaji hayaruhusiwi kufanyiwa kitu chochote mbadala ya kilichoelekezwa na Serikali hivyo si busara kwa mtu kujichukulia eneo bila ruhusa kutoka mamalaka husika.

Awali sheha wa Shehia ya Kiuyu Minungwini Yahya Salim Amir ambaye eneo lake la Chamanangwe linalomilikiwa na wizara ya kilimo limejengwa nyumba tano na kutumika kwa kilimo  amewashauri  wananchi kukubali kufanyiwa tathmini ya mali zao na kuhama ili kuiwachia Serikali  kufanya shughuli zake.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib amesema watahakikisha kuona maeneo hayo yaliyotengwa  hayatumiwi vibaya .

Comments