RC Kaskazini Pemba awapa neno madaktari wa kichini Kisiwani Pemba.


 
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh.Omar Khamis Othman ,ameipongeza timu ya tano ya madaktari wa Kichina kwa kwazi nzuri wanaoifanya huko maabara ya kichocho  mkoroshoni kwa kuendelea  kutoa huduma za matibabu Kisiwani Pemba kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa huo ambao unaendelea kuathiri wananchi .

Kauli hiyo ameitoa huko Maabara ya kichocho Mkoroshoni wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa serikali kutoka Wizara mbali mbali za Pemba kwa lengo la kujua maendeleo ya mradi huu wa kutibu kichocho unaofadhiliwa na serikali ya kichina ili kuweza kutoa ushirikiano  katika utendaji  wa kazi kwenye shehia zilizoingia kwenye mradi huo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kazi kubwa iliyombeleyao nikuwahamasisha wananchi kuata maelekezo yanayotolewa na watalamu hao kuona ugonjwa huo unaondoka kwa wananchi unguja na Pemba .

Hata hivyo alimtaka kiongozi wa timu hiyo kumuomba balozi wao wa China aliyepo Zanzibar kumuomba Rais kuwatembelea kuangalia kazi wanazonzifanya na hatua waliofikia kwa utoaji wa matibabu ya ugonjwa huo.

Nae Mkuu wa kitengo cha kichocho Pemba Saleh Juma Muhammed, alisema lengo la Mradi huo nikuondosha Ugonjwa huo na kwa hatua ya kwanza ni kuwauwa konokono kwa kuwatia dawa mitoni ambako ndio kwenye mazalia yao.

Alifahamisha kwamba waliamua kulifanyia kazi eneo la Uwandani kwa majaribio kwani ndio eneo kubwa lilokuwa limeathirika hapo awalikuwavasilimia 8.59  kiwangon hicho ni kikubwa na sasa tumefikia asilimia 0.6  baada ya kuwapima watu zaid ya 100 ambao waligundulika  wanaugua kichocho.

“kwa kweli tukipoanza kuingia kijiji cha uwandani ilikuwa hali ni mbaya lakini kwa mashirikiano ya wananchi viongozi wa shehia tumefanikiwa na lengo tumefikia” alisema.

Aidha alifahamisha kwamba baada ya kupatamafanikio kijiji cha Uwandani ambako tuliweka kama majaribio kuna vijiji vyengine nako tunatoa matibabu  amboko ni Mtangani,na Wingi huko kuna tatizo la ugonjwa huo.

Kwa upande wake kiongozi wa timu ya madaktari hao Dr, LUANG YUZHENG, alisema  serikali ya China kwa kuendelea kwa mara nyengine ya mradi wao kwa kuwasaidia wananchi wa Pemba na Unguja kwani ugonjwa huo umekuwa ukiathiri  ugonjwa huo.

Alifahamisha Ugonjwa huo huambukizwa na Konokono ambae huzaa vimelea milioni moja kwa wakati mmoja kwenye mto  kusema idadi  hiyo ni kubwa  ambapo isipochukuliwa hatua  wananchi wataendelea kuathirika.

Alifahamisha kwamba matarajio nikupata mafanikio kulitokomeza gonjwa hilo kama walivyofanikiwa katika nchi yao kwani wananchi wengi nako wanaathirika kwa matumizi mabaya ya maji katika mito .

Kwa Upande wake afisa Mdhamini wa Wizara ya afya Pemba Shadya Shaaban Seif, alisema Wizara yake imekua ikitoa mashirikiano makubwa na madaktar hao pamoja  wakuu wa kitengo cha kumbambana na ugonjwa huo .

Hata hivyo alifahamishakwamba  wataendelea kuwaelimisha wananchi juu athari ya ugonjwa pamoja na kutia dawa kwenye maziwa.

Afisa Elimu Mkoa Kusini Pemba Mwalimu haji Kombo, alisema   baada ya kuona kazi zinazofanywa na madaktari hao maabara ya Kichocho atawahamasisha walimu wezake kuelezea athari za ugonjwa wa kichocho kwani kuna masomo maalumu wanayosomesha katika skuli zao na kusema watapata fursa ya kuwapeleka wanafunzi hao kusoma na kujua zaidi ugonjwa huo .

Nae Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Rashid Hadidi Rashid, alisema ataendelea kuzungumza na masheha wake kwenye mikutano yao ili kuweza kuelimisha jamii ndani ya shehia zao wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo na kuacha matumizi ya maji kwenye mito na kutunza mazingira hatarishi ambayo yanachangia maambukizi .

Comments