KAMATI ya Baraza La Wawakilishi ya Ustawi wa Jamii imetembelea
kituo cha damu salama kilichop Wete katika Wizara ya afya Pemba kuangalia
shughuli za maendeleo kwa kituo hicho na utoaji wa huduma kwa
wananchi pamoja na kujua changamoto zinazowakabili watendaji hao.
Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa
wizara ya afya huko ofisi kuu ya Wizara Wete Pemba Makamo mwenyekiti wa
kamati hiyo Nassor Salum Ali, ambaepia ni mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni
,amesema suala la uchangiaji wa damu salama ni muhimu sana na kusema
ameridhishwa na juhudi zinazochukuliwa na watendaji wa wizara na kusema
changamoto watazifanyia kazi zinazowakabili kituoni hapo.
Amefahamisha kuwa rais wa Zanzibar dr.Ali Muhammed
Shein, amekuwa akifanya kazi vizur na kuiyunga mkono Wizara ya afya kwa
kuboresha huduma muhimu kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu wananchi wake.
Nae Mjumbe wa kamati hiyoYussuf Hassan Iddi,ambae
pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni amewaomba viongozi na wafanyakazi wa wizara
hiyo pemba kufanyakazi kwa mashirikiano ili kuona mafanikio yanaimarika
zaidi kwa utoaji wa huduma zilo bora .
Kwa upande wake afisa Mdhamini wa Wizara ya
afya Pemba Shadya Shaaban Seif , ameishukuru kamati baraza la Wawakilishi
ya Ustawi wa Jamii kwa kuwaunga mkono na kusema imesaidia kuwatatulia
changamoto tangu kuanza kutembelea mara kwa mara kisiwani pemba.
Akitoa maelezo kuhusu uwendeshaji wa kituo hicho
Mkuu wa kitengo cha Damu salama Pemba ,Abdi Kassim Hamadi, amesema
licha ya mafanikio makubwa waliyopta tangu kuanzisha kituo hicho pemba
wanakabiliwa na changamoto ya kifaa cha utoaji wa majibu ya damu baada ya
uchangiaji na kulazimika kuzipeleka Ofisi kuu Unguja iliyopo Amani kwa
uchunguzi na kutolewa majibu ya damu hizo nakuwaomba kupatiwa japo mashine
ndogo itakayoweza kutoa majibu kwa haraka.

Comments