
Wafanyakazi
wa sekta zilizogatuliwa Mkoa wa Kusini Pemba wameimuomba serikali kuwaongezea
wahudumu na vitendea kazi ili
kufanikisha majukumu yao kwa ufanii zaidi.
Wamesema
sekta hizo zimekuwa na changamoto ya kiutendaji ikiwemo uchache wa wafanyakzi
na wengine kufikia umri wa kustaafu.
Hayo
wameyasema kwa nyakati tofauti mbele ya Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali
za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mheshimiwa Haji Omar Kheir kwenye mikutano ya
kusikiliza matatizo yanayozikabili sekta zilizogatuliwa Kisiwani Pemba.
Wamesema
katika kuona maendeleo yanazidi kuimarika ni vyema kwa serikali kubuni nafasi
zaidi za ajira na kuzitafutia ufumbuzi
changamoto ndogo ndogo zilizopo.
Katika
ziara hiyo waziri afisi ya rais tawala za mikoa serikali za mitaa na idara
maalum za smz Mheshimiwa Haji Omar Kheir amesema kwa kushirikiana na viongozi
wengine watakaa kuyafanyia kazi matatizo yaliopo ili kuona sekta hizo zinasonga
mbele kama ulivyo mpango wa serikali wa kuwaletea wananchi wake huduma karibu
nao .
Amesema
katika kuimarisha dhana ya ugatuzi serikali imepanga katika bajeti ya
2019-2020 kujenga madarasa 600 unguja na pemba ili kukidhi haja ya
ukosefu wa vyuma vya kusomea.
Mapema
mkuu wa mkoa wa kusini pemba mheshimiwa hemed suleiman abdalla amewataka
wafanyakazi hao kuzidi kujituma huku serikali ikiendelea kuzitafutia ufumbuzi
wa kina changamoto zao.
Comments