Hospitali ya Wete na Micheweni Wapewa Msaada wa Mashuka.


Mbunge wa bunge la Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania wa viti maalum CCM UWT wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Maida Hamad Abdalla, amekabidhi mashuka 100 kwa hospitali ya Wete na Hospitali ya Micheweni  kwa Wodi ya Mama na Mtoto ambapo kila hospitali itapata Mashuka 50 ambayotapunguza upungufu wa matatizo hayo.

Umoja wa UWT wa Mkoa wa Kaskazini umeamua kutoa msaada wa mashuka hayo kwa hospitali mbili kwa wodi ya akina mama na watoto kwa kuona umuhimu mkubwa kutokana na mazingira yao kwani kunahitajika usafi wa mara kwa mara.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kumkabidhi Mashuka hayo afisa mdhamini  wa Wizara ya Afya hapo hospitali ya Wete ,alisema kuwa lengo kuu la kutoa ni kutekeleza ilani ya CCM ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 katika kuhakikisha wanaboresha huduma ambazo zimeanishwa kwenye ilani hiyo.

Mbunge huyo alisema kuwa wameona ipo haja kutoa msaada huo ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kutimia miaka 42 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi ambapo ndio maana ya kutoa msaada huo .

Aidha ameipongeza Wizara ya afya kwa kuborsha huduma kwa kujenga vituo vya afya kwa kuwasogezea wananchi wake huduma pamoja na dawa za mmatibabu bure.

“Kwa kweli serikali yetu imekuwa ikiongeza bajet kubwa kwa kuhakikisha wanaboresha huduma mbali mbali kwenye Wizara zake ili kufikia malengo ya ilani yetu ya Uchaguzi”.alisema Mbunge huyo.

Akipokea msaada huo Afisa Mdhamini wa Wizara ya afya Pemba Shadya Shaaban Seif, amemshukuru Mbunge huyo wa Umoja wa akina mama wa Mkoa wa Kaskazini kwa uwamuzi wake kwa kutoa mashuka 100 ambayo yatatumika kwa wodi ya mama na watoto kwa kuonyesha kuwa jali wananchi wake.

Aidha alisema msaada huo umekuja wakat muafaka kwani hospitali ya Wete imekuwa ikipokea  wagonjwa wengi ambaob wanalazwa na kusema watayatumia kama ilivyo kusudiwa na kuwataka wahisani wengine kusaidia .

Nae mwenywkiti wa Mkoa Kaskazni Pemba Miza Khamis Haji ,aluwomba uwongozi wa hospital ya Wete na Micheweni kuyatunza mashuka hayo  ilikudumu zaidi  pamoja na kuthamini michango ya wafadhili wanayoitoa.

Kwa upande wake afisa uwendeshaji Tiba  wa Wizara ya afya Pemba Dokta Yussuf Hamad Idi, aliwataka madaktar dhamana walokabidhiwa mashuka hayo kwa hospitali mbili hizo  kuhakikisha wanayatumia ipasavyo ili malengo ya msaada huo ufanikiwe kwa matumizi yalokusudiwa.

“Nakuombeni wafanyakazi na madaktar mliokabidhiwa mashuka hayo yatumike kama ilivyotakiwa nitakapo baini mashuka hayo sito mfumbia macho muhusika atakae kwenda  kinyume na msaada huo  hatua za kisheria zitafata juu yake”. alisema.   

Wakitoa neno la shukurani mbele ya Mbunge huyo kwa niaba ya madtar wafanyakazi wengine wa hospital hizo  mbili dokta dhama wa wete Omar Issa Mgongo , alisema wameupokea msaada huo na kuahidi kutumia kwa malengo yalokusudiwa.

Comments