Waziri wa Elimu Zanzibar afungua kituo cha huduma za kinga na tiba ya mifungo fuoni.

Image may contain: 4 people, people sittingWAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwaunga mkono wananchi na wafugaji kwa kuwapatia huduma bora za kinga na tiba.

Akizungumza wakati alipofungua kituo cha huduma za kinga na tiba ya mifungo huko fuoni wilaya ya Magharib “B” ikiwa ni shamra shamra ya kusherehekea miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe Riziki amesema Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi imepewa jukumu La kuendeleza sekta hizo ikiwemo mifugo, hivyo itaendelea kuwahamasisha wafugaji kufuga kibiashara ili kujiongezea tija na mapato zaidi.

Amefahamisha kuwa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, itaendelea kuwapatia wafugaji ushauri wa kitaalamu kuhusu ufugaji bora wa kisasa kwa lengo la kuinua hali za maisha na kupunguza umaskini nchini.

Aidha, amewataka wanachi kukitumia vizuri kituo hicho na kukitunza ili kiweze kuwasaidia katika kuwapatia huduma bora za kisasa kwa ajili ya wanyama wao.

Hata hivyo amewashauri wananchi kuwa na utamaduni wa kufuga wanyama aina ya sungura kwani wameonekana kuwa na faida kubwa kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla.

Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Bw Ahmed Khamis kupitia risala yake amewataka madaktari wa wanyama kuendelea kufanya kazi zao kwa bidii zaidi na kuwashauri wafugaji kuzitumia fursa zilizopo ili kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa nchi.Image may contain: 16 people, people smiling, crowd and outdoorImage may contain: 2 people, crowd and outdoor

Comments