Akifungua mradi wa maji safi na salama katika kijiji cha Donge Mbiji
ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 55 ya mapinduzi, alisema
lengo ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.
Aidha alisema pamoja na kujitokeza kwa changamoto za uharibifu wa
mazingira kwenye vianzio vya maji safi na salama, serikali ipo makini na
inafanya juhudi kuhakikisha huduma hiyo inakuwa endelevu.
Mapema Katibu Mkuu Wizara, Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Alhalili
Mirza, alisema mradi huo umegharimu dola za Marekani milioni 5.5
ambapo kwa Donge zimetumika dola za Marekani 1.8 milioni.
Alisema serikali imechangia shilingi milioni 513 kwa ajili ya malipo ya fidia na uvutaji wa umeme.
Aidha alisema mradi huo ni msaada kutoka serikali ya China na
unatarajiwa kuwanufaisha watu 102,000 ambapo upande wa Donge ni watu
48,000.
Alitaja maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo kuwa ni pamoja na Chaani, Kisongoni, Kiboje na Miwani.
Katika hatua nyengine alisema kazi zitakazotekelezwa kupitia mradi
huo ni pamoja na uchimbaji wa visima, ujenzi wa matangi,mitambo ya
kutilia dawa na ulazaji wa mambomba.
Alisema utekelezaji huo unaenda sambamba malengo ya dunia (SDG), dira
ya maendeleo ya taifa 2020, Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza
umasikini Zanzibar (MKUZA III) na ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020.
Nae Balozi mdogo wa China Zanzibar Xie Xiao Wn, alisema serikali ya
China inashukuru kuamini na Zanzibar katika uendelezaji wa ujenzi wa
miradi ya maendeleo kwa ajili ya wananchi.
Mkandarasi wa mradi huo kutoka China, Shein Qi alisifu juhudi
zilizochukuliwa katika utekelezaji wa mradi huo huku akiahidi
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama endelevu.
Zanzibarleo.
Comments