WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amezindua tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa
na kuushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuwa tawi hilo litahamasisha
ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi kujua umuhimu wa
kuhifadhi fedha zao benki.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan
kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya
wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea
umbali mrefu.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo jana (Jumatatu, Desemba 31, 2018) wakati
akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuzindua tawi
la benki ya CRDB, ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamisha wananchi
kutumia benki kwa kuhifadhi fedha zao.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema kwa sasa benki hiyo inatakiwa itoe mikopo
midogo, ya kati na mikubwa kulingana na uhitaji wa wajasiriamali ndani
ya wilaya hiyo kwa sababu mikopo itawawezesha wananchi waweze kukuza
mitaji na kujikwamua kiuchumi.
Pia
Waziri Mkuu ameipongeza benki ya CRDB kwa kumuunga mkono Rais Dkt. John
Magufuli katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo za
afya pamoja na elimu kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na benki
hiyo nchini.
Awali,
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki
ya CRDB imekua na kupanua wigo wake wa kufikisha huduma kwa wateja na
kuunga mkono sera ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wengi zaidi
wanapata huduma za fedha.
Alisema
tawi hilo ni la sita katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania, kwani tayari
wanamatawi mengine manne ambayo ni Lindi mjini, Mtwara, Masasi,
Tandahimba na tawi linayotembea katika Wilaya ya Newala. Pia wapo
katika hatua za mwisho za ujenzi wa tawi Nachingwea.
“Wilaya
hii ya Ruangwa ni kiungo muhimu sana katika uchumi wa mkoa wa Lindi na
Taifa kwa ujumla, hivyo uwepo wa mfumo rasmi wa kibenki, kupitia tawi
hili la Benki ya CRDB, utasaidia sana kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi
kwa kufungua fursa mpya.”
Mkurugenzi
huyo alisema CRDB wanajivunia utendaji mzuri wa tawi hilo, kwani katika
kipindicha mwaka mmoja toka limeanza kazi, limeweza kupata matokeo
makubwa ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa amana ambazo
zimefikia kiasi cha shilingi bilioni 1.5.
Pia
jumla ya AMCOS 12 wanachama 4,600 zimejiunga na kufungua akaunti zao
hivyo kuongeza usalama wa fedha zao. Pia jumla ya mikopo ya shilingi
bilioni 1.2 imeshatolewa kwa wateja wa wilaya hiyo, ambapo shilingi
milioni 409 zilitolewa katika kilimo cha korosho na ufuta, wakati
shilingi milioni 790 zilitolewa kama mikopo kwa wafanyakazi na
wafanyabiashara.
Mpekuzi.
Comments