Hatimaye
wananchi wa shehiya ya sizini na vijiji vya jirani wameanza kupata huduma ya
afya ya mama na mtoto baada ya kufunguliwa jengo la kituo cha afya katika
shehia hiyo.
Kituo
hicho kinatarajiwa kutoa huduma kwa watu wapatao elfu tano (5000) kimejengwa
kwa msaada wa zanzibar milele foundation na kuwa na uwezo wa kutoa huduma ya kujifungulia akina mama
wajawazito.
Akifungua
kituo hicho huko Sizini Wilaya ya Micheweni katika shamrashamra za miaka 55 ya Mapinduzi
ya Zanzibar mjumbe wa baraza la mapinduzi na waziri wa vijana utamaduni sanaa
na michezo Balozi Ali Karume amewataka wananchi kukitumia kituo hicho kwa dhamira
iliyokusudiwa ikiwemo akinamama kujifungulia ili kuimarisha viwango vya afya
yao na watoto wao.
Amesema
katika kuyaenzi na kuyalinda mapinduzi hayo ni lazima kila mmoja kuwajibika kwa
nafasi yake katika kuleta maendeleo
ikiwemo kujenga na kuvitumia vituo vya afya ili kuwa na afya bora
Mapema
Afisa Miradi wa Zanzibar Milele Foundation Pemba Fatma Khamis Silima amesema ujenzi kituo hicho
kilichogharimu shilingi milioni mia nne kimejengwa kwa mahitaji maalum
kutokana wananchi wa sizini kuwa na kituo kidogo cha afya na akina mama kwenda micheweni ambako nimbali
kupata huduma ya kujifungulia.
akitoa
salamu za wilaya ya micheweni kwa balozi ali karume mkuu wa wilaya hiyo salama
mbarouk khatib amesema wilaya ya
micheweni na wananchi wa sizini wamefarajika kwa kukabidhiwa kituo ambapo
kitaondoa usumbufu mkubwa wa kufuata matibabu masafa marefu.
Comments