Wanakijiji cha Mzuri Makunduchi waiomba paza kuwasaidia zaidi.


Mwanakijiji wa shehiya ya Mzuri kilichopo makunduchi Rashid Haroun Rashid (29) amewaomba wasimamizi wa Mradi  wa PAZA kusimamia  ujenzi wa skuli ya maandalizi mara baada ya kukamilika   ukarabati wa vyoo vya skuli ya Kusini Unguja.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Muandishi wetu ameeleza kwamba  Mradi wa kukuza uwajibija Zanzibar (PAZA) umefanikiwa kupunguza matatizo mengi katika wilaya ya kusini Unguja ikiwemo tatizo utoro na uzalilishaji  kwa wanafunzi, uchakavu wa jengo la skuli pamoja na ukosefu wa maji safi na salama katika wilaya hiyo.

Hata hivyo amesema hana budi kuushukuru Mradi wa PAZA kwa kuwaondolea shida ya maji katika eneo hilo kwani wananchi wameridhika kwa kupata maji safi na salama japokua yanatoka kwa mgao lakini wanaamini mradi ukiendelea maji yatapatikana yakutosha kwa wananchi wa kusini unguja.

Nae Bi Zawadi Hamdu Vuai (53) mkaazi wa shehia ya Mzuri amesema katika Mkoa wa Kusini  kwa sasa utoro na vitendo vya udhalilishaji kwa wanafunzi vimeondoka, majengo ya skuli yameboresha na walimu wameongeza kwa kila skuli ambayo iliyokua na uhaba wa walimu.

Aidha amesema baada ya mradi wa PAZA kuwahamasisha  wananchi njia za kutatua matatizo yanayowakabili katika maeneo wanayoishi, ambapo vijana  wa shehia ya Mzuri, Nganani na Kajengwa wamechukua hatua   kufuata watoto watoro majumbani mwao na kuwapeleka skuli hali iyopelekea kupunguza utoro maskulini.

Naye afisa elimu kusini Unguja  Haji Mohamed Abdulla akijibu suali la mwandishi aliyetaka kujua mfumo wa ufundishaji wanafunzi amesema wataendelea na Uwajibikaji kwa wanafunzi kwa kutoa huduma bora  na kuhakikisha ufundishaji unafanyika kwa kufuata mtaala ulioandaliwa na wizara ya elimu Zanzibar.

Hivyo amesema ofisini yake itaendelea na utaratibu wa kusimamia majengo ya skuli kuwa safi na mazima pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika  mazingira bora na salama.

Mradi wa kukuza Uwajibikaji Zanzibar (PAZA) ulianza mwaka jana kwa lengo la kukuza Uwajibikaji Zanzibar ili kuwahamasisha wananchi njia za kutatua matizo yanayozunguuka katika jamii na utarajiwa kumalizika  mwakani.



Na RAHMA MOH’D

Comments