Ufaransa
imepinga matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, ikisema ushindi uliotangazwa kwa kiongozi wa upinzani, Felix
Tshisekedi haulingani na matokeo ambayo mpinzani wake mkubwa, Martin
Fayulu anaonekana kuupata.
Katika
tamko lililotolewa jana baada ya matokeo ya awali kutangazwa, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian alisema Fayulu, ambaye
alitangazwa kushika nafasi ya pili, ndiye aliyetakiwa kutangazwa
mshindi.
"Kwa
kweli inaonekana matokeo yaliyotangazwa, hayaendani na matokeo halisi,"
alisema alipozungumza na kituo cha televisheni cha CNews.
"Kwa kuangalia (matokeo halisi), Fayulu ndiye kiongozi aliyepatikana katika uchaguzi huu. "
Alisema
Kanisa Katoliki, ambalo lina wafuasi wengi na ambalo lilituma
waangalizi 40,000, linajua nani hasa aliyehinda na maoni yao yanaonyesha
mshindi ni Fayulu.
"CENCO
ilifanya ukaguzi na kutangaza matokeo ambayo yalikuwa tofauti," alisema
akimaanisha baraza la maaskofu la Kanisa Katoliki.
Comments