Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Congo (Ceni) imetangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo yanayoonesha mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi ameshinda kiti cha Urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Desemba 30 mwaka uliopita.
Tshisekedi
amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na
mgombea aliyekuwa anaungwa mkono na serikali ya Rais anayemaliza muda
wake, Emmanuel Shadary.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa,
mapema leo Alhamisi amesema kwamba kwamba Bw Tshisekedi amepata asilimia
38.57 ya kura zilizopigwa na kumtangaza rasmi kuwa Rais mteule wa nchi
hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini na mafuta.
Tshisekedi
anatokea katika muungano wa kisiasa na aliyekuwa mgombea wa chama cha
UNC (Union for the Congolese Nation), Vital Kamerhe ambaye atakuwa ni
Waziri Mkuu wa serikali yao kwa mujibu wa makubaliano yao.
Ripoti
zinaeleza kuwa mshindi wa kwanza (Felix Tshisekedi) amepata kura
takriban milioni 7, huku mshindi wa pili (Martin Fayulu akipata kura
takriban milioni 6.4 milioni na mgombea wa tatu ambaye anaungwa mkono na
Rais Joseph Kabila (Emmanuel Ramazani Shadary) akipata takriban kura
millioni 4.4.
Comments