Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Mrajisi wa elimu Zanzibar, Hashir Mussa
Mzee, huko , ofisini kwake Vuga.
Alisema, kuna gari za baadhi ya skuli zinajaza wanafunzi kinyume na uwezo wa gari jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.
Alisema hivi karibuni Kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharibi,
Thobias Gesaude, alizungumza na wamiliki wa skuli binafsi juu ya umuhimu
wa kulinda usalama wa wanafunzi ndani ya gari.
Hivyo, aliwasisitiza kuacha tabia hiyo na kuhakikisha wanafunzi wote
wanakaa juu ya viti ili kuwaepusha na matatizo mbalimbali yanayoweza
kuwapata.
“Wazee wanalipa ada ya usafiri kila mwaka kwa ajili ya mtoto kupata
huduma nzuri, sasa kuwajaza kupita kiasi na watoto wengine kusimama hiyo
si haki,” alisema.
Alibainisha kuwa, skuli yoyote itakayoonekana inakiuka amri zinazotolewa na wizara, itachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
“Zipo adhabu ikiwemo kifungo na faini kwa mtu atakayekwenda kinyume
na sheria ya elimu, kwa hivyo wanaopuuza sheria tutawachukulia hatua,”
alisema.
Hata hivyo, alisema wizara ipo katika mchakato wa kurekebisha sheria
hiyo ili kuhakikisha adhabu kwa wakosaji inakuwa kali zaidi.
Comments