Aliyewahi
kuwa Mbunge wa Maswa kupitia CCM, na Maswa Magharibi, John Shibuda
amesema Muswada wa Vyama vya Sheria unaotarajia kupelekwa bungeni
unaidhalilisha CCM.
Akizungumza
jana katika mdahalo wa vyama vya siasa, Shibuda kwa sasa ambaye ni
Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya Siasa visivyo na uwakilishi bungeni,
alisema CCM kama mzazi wa vyama vingi havipaswi kukandamiza vyama hivyo.
Akifafanua
kuhusu kifungu kinachozuia viongozi kuhama vyama na kupewa nafasi za
kugombea, Shibuda alhoji kwanini mwanachama azuiwe wakati ni uhuru wake
na chama chake kufanya hivyo.
"Unamuogopa
nani?, Inamaana ukihama dini moja labda umetoka Uislam kwenda Ukristo
usioe mpaka mwaka upite?. Kasema nani? Sheria hii inaidhalilisha CCM.
Nawaombeni mnaokwenda kutegeneza sheria mkazijadili kwa kina" Shibuda.
Aidha
aliongeza kwamba, "Mzazi wa vyama vingi ni CCM na mlezi wake ni
serikali. Sasa mzazi ukizaa mtoto ukamuacha akiwa chokoraa akikutukana
usilalamike. Tengenezeni tafsiri ya huu muswada. Chama cha siasa
kinapaswa kukonga nyoyo za wananchi na siyo kutegemea kuua chama
kingine".
Mpekuzi.
Comments