Wizara
ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikia na kampuni ya O2 and B imetoa
mtambo maalum wa kupunguza kiwango cha madini ya ‘fluoride’ kilichozidi
kwenye maji yanayotumiwa na wananchi wa kijiji cha Lemanda, kata ya
Oldonyo Sambu wilayani Arumeru.
Mtambo huo, umefanyiwa majaribio na wataalamu wa kampuni hiyo kutoka China ambao wanatengeneza mitambo huo.
Akizungumza
wakati wa kusimika mtambo huo, zoezi lililofanyika katika Shule ya
Msingi ya Oldonyo Sambu, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Arusha, Dk.
Wilson Mahera, alisema wamepokea mtambo huo kutoka serikali kuu kupitia
Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Mtambo
huo unaojulikana kwa jina la “Capacity of Deionization System,” (CDI),
mtambo huo una uwezo wa kuchuja maji kwa kiwango kikubwa na kupunguza
kasi ya madini ya fluoride kwenye maji.
“Mtambo
huu una uwezo mkubwa wa kupunguza kiwango cha madini ya fluoride
kilichozidi pamoja na chumvi chumvi kwenye maji, kwa kutumia teknolojia
hii ya kisasa ya kuchuja maji bila kutumia kemikali kitapunguza madhara
kwa wananchi wetu,” alisema.
Alisema
mtambo huo una uwezo wa kuchuja maji na kupunguza kiwango cha fluoride
kutoka miligramu 18.7 kwa lita moja hadi kufikia miligramu 0.37 kwa lita
moja.
“Matarajio
ya serikali ni kukabiliana na tatizo hii na litamalizika na kutoa
matumaini mapya kwa wananchi wa Lemanda ya kutooza meno na kupinda miguu
kutokana na matumizi ya maji yenye madini ya fluoride,” alisema Mahera.
Mpekuzi.
Comments