Samia aitaka TAWJA isaidieni upatikanaji haki.

MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wanawake nchini kutoyumba katika kudai na kupigania haki zao, hasa ikizingatiwa kuwa serikali imeweka mazingira rafiki ya kisheria.
Kauli hiyo ameitoa katika hoteli ya Verde alipokuwa akifungua mkutano wa tisa wa Chama cha Majaji Wanawake nchini (TAWJA), ambapo alisema wanawake hawapaswi kuyumba katika kudai haki zao.
Alisema miongoni mwa miundombinu rafiki ya kisheria ni pamoja na kuridhia mikataba ya kimataifa ambayo inatoa usawa wanawake kudai haki zao.
Alikitaka chama hicho kinachojumuisha majaji, mahakimu na maofisa wa sheria wanawake kuhakikisha kinawapa fursa wanawake kudai haki zao kisheria sambamba na kuchangia uchumi wa nchi.
Samia alisema kuwepo kwa chombo hicho kutaweza kuimarisha usawa kwa jinsia zote ili kuona haki zinatekelezwa kwa watu wote.
Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma alisema chama hicho kimekuwa mstari wa mbele kuisaidia mahakama katika kuhakikisha kinaendeleza usawa kwa wanawake kwa kuwaelimisha juu ya haki zao na pia kuweza kushirikiana na mashirika ya kimataifa kukuza usawa huo.
Aidha aliziomba mahakama kurekebisha baadhi ya sheria zao ambazo zitawakwamua wanawake katika kusimamia vyema majukumu yao.
Prof. Juma alisema mahakama kuu ya Tanzania inakitambua chama hicho kwani kimekuwa kiungo muhimu na kutoa fursa katika kutatua kero za wanawake zinazohusu sheria.
Kwa upande Mwenyekiti wa jumuya Majaji wanawake Tanzania Jaji Imani Daud Aboud, alisema chama hicho kimepatia kuwa haki sheria za wanawake zianapatikana nchini kote ili kujua wanawake wnapata haki zao nchini kote.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa Zanzibar, Jaji Fatma Hamid Mahamoud alisema wanafanya kazi kikamilifu katika kuhakikisha wanawake wanapata haki zao za msingi katika kupigania vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia nchini.
Mkutano wa chama cha majaji wanawake Tanzania TAWJA ni wa siku tatu ukiwa na lengo kubwa la kuwkomboa wanake nchini.

Comments