RC Makonda Amuombea Msamaha Tundu Lissu....Amtaka Spika Ndugai kumpeleka milembe atakaporejea nchini.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewaomba watanzania kumsamehe
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu kwa kauli anazozitoa
huko nje ya nchi.
Makonda
ametoa kauli hiyo leo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
John Pombe Magufuli, katika Mkutano wa Wachimbaji, Wafanyabiashara na
Wadau wa sekta ya madini nchini.
Makonda
amesema kwamba amegundua kwamba kauli za Lissu zinatokana na kwamba
bado hajapona vizuri kichwani kutokana na yeye mwenyewe kukiri wakati
alipokuwa akimaliza mahojiano katika kipindi cha 'Hard Talk'
kilichofanyika jana na kituo cha televisheni cha BBC.
Ameeleza
kwamba katika mahojiano hayo, Lissu ameshindwa kujibu juhudi za
Magufuli namna anavyopigana katika suala la madini, ambapo aliikimbia
mada hiyo na kuzungumzia mambo mengine ya tofauti, hivyo inaonyesha
bado anaendelea kupokea malipo.
"Kama
bado mgonjwa inamaana kichwani mambo hayajaakaa vizuri na ndo maana
anahitaji matibabu na akitoka kule, tunamuomba Spika amfikishe Mirembe
pale na aendelee kumuhudumia".Amesema Makonda
Comments