Rais
John Magufuli ameweka wazi kwamba hafurahishwi na migogoro kati ya
viongozi anaowateua na kusema kuwa amewaweka kiporo Mkuu wa Wilaya na
Mkurugenzi wake kutokana na matendo yao ya kugombana badala ya kufanya
kazi hivyo wasifikiri kwamba hafahamu.
Rais
Magufuli ameyasema hayo jana baada ya kumaliza kuapisha viongozi wapya
aliowateua baada ya kufanya mabadiliko katika Wizara mbalimbali pamoja
na Makatibu wa Wizara.
Rais
alisema kwamba anafahamu changamoto ni nyingi katika utendaji wa kazi
ingawa yapo mengine mazuri wanayofanya na kuwataka wahakikishe wanajitoa
kwa maslahi ya wananchi.
"Nafahamu
hizi kazi zina changamoto nyingi sana mfano kuna DC Gairo na Mbunge
hawaelewani mpaka Mbunge anapost kumtukana DC tena mke wa mtu, hajui
kama anaweza upoteza Ubunge, "I hope' siku moja ataomba msamaha kwenye
Bunge", alisema Mh Rais Magufuli na kuongeza;
"Halmashauri
ya Nyasa wanagombana sana DC na Mkurugenzi, nimewaangalia tu!
nimewaachia kiporo chao. Pale Dodoma Mkurugenzi wa Jiji na DC walikuwa
wanagombana nika-send meseji nikawaambia endeleeni kugombana siku moja
mtagombania Vijijini, wamenyamaza naona yameisha".
Mpekuzi.
Comments